CHANGAMOTO YA MSONGO WA MAWAZO YAMPOTEZA KIJANA DOTTO CHACHA – KILOLENI, TABORA

Katika siku za hivi karibuni, tumepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya msiba mzito uliotokea Kiloleni, Manispaa ya Tabora – ambapo kijana mwenzetu Dotto Chacha alipoteza maisha kwa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo.
🖤 Tukio hili limetuacha na majonzi, lakini pia linatufungua macho juu ya uhalisia wa changamoto za afya ya akili, hususani kwa vijana.
✳️ Dotto alikuwa nani?
Dotto Chacha alikuwa kijana mchapakazi, mwenye ndoto na matumaini. Lakini kwa bahati mbaya msongo wa mawazo kutokana na kupata majeraha mbali mbali sehemu ya mwili wake baada ya kupata ajari. Kumpelekea kufanya maamuzi magumu na yakuhudhunisha.
---
🟢 Kwetu, tunasimamia haya:
✅ Kuhamasisha jamii kusikiliza zaidi kuliko kulaumu
✅ Kujenga utamaduni wa mazungumzo ya wazi kuhusu afya ya akili
✅ Kuelimisha mashuleni, mitaani na kwenye majukwaa ya kidijitali kuhusu namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo
✅ Kutoa nafasi kwa vijana kupata msaada wa kitaalamu au wa karibu kupitia kampeni zetu
---
🕊️ Tunatoa pole nyingi
Kwa familia ya Dotto, marafiki, jirani na jamii yote ya Kiloleni – tupo pamoja nanyi.
Tukio hili liwe mwanga mpya wa sisi kama jamii kuona, kuelewa, na kusaidia kabla ya kuhukumu.
🟢 Kama una changamoto yoyote ya kisaikolojia au unajisikia kupotea, tafadhali zungumza na mtu, tafuta msaada. Upo kwa thamani. Tupo kwa ajili yako.
---
ELIMIKA. CHUKUA HATUA.
KWETU – Tabora. Tanzania.
Tags:
simulizi