🤝 Tunachofanya
Tunakusanya simulizi za maisha halisi kutoka kwa vijana mashujaa wa Tabora na Tanzania kwa ujumla – hadithi zinazogusa moyo, kuelimisha na kuhamasisha.
Tunatengeneza content zenye tija na kuelimisha kupitia mitandao ya kijamii, video fupi, podcast, na machapisho ya majarida kwa lugha ya Kiswahili inayofikika kwa kila mmoja.
Tunaandaa kampeni, mashindano, na michezo ya kidigitali kama njia ya kuvutia na kuhamasisha ushiriki wa vijana katika mambo ya kijamii na kiuchumi.
Tunatoa elimu ya kivitendo kwa vijana, hususan katika nyanja za ujasiriamali, afya, teknolojia, mazingira, na malezi bora.
Tunawezesha vijana kiuchumi kupitia mafunzo ya stadi za maisha, miongozo ya biashara ndogo ndogo, na ushauri juu ya kuanzisha miradi endelevu.
Tunashirikiana na shule, vikundi vya vijana, na taasisi nyingine kuendesha semina, warsha na makongamano yanayolenga kukuza maarifa na kuwajengea vijana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
Tunatambua na kuinua vipaji kwa kutoa majukwaa ya kujieleza kupitia sanaa, muziki, michezo, na ubunifu.