"Mtoto Salama, Familia Salama"
> Mwongozo kwa Wazazi: Jinsi ya Kuweka Watoto Salama Ukiwa Kazini


🟩 Uk. 1 - Utangulizi

Neno kutoka 'Kwetu':
Katika ulimwengu wa leo wa mihangaiko na majukumu ya kila siku, wazazi wengi hulazimika kuwa mbali na watoto wao kwa muda mrefu wakiwa kazini. Lengo la jarida hili ni kutoa maarifa na mbinu rahisi za kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama, wenye malezi bora na mwelekeo mzuri hata tunapokuwa mbali nao.-

🟩 Uk. 2 - Changamoto Zinazowakumba Watoto

Kukosa uangalizi wa karibu
Kuathirika kisaikolojia (upweke, hofu, huzuni)
Hatari za unyanyasaji (kimwili, kingono, au kihisia)
Matumizi mabaya ya simu na intaneti
Kukosa mwelekeo wa muda na kazi


🟩 Uk. 3 - Mbinu kwa Wazazi Kuwalinda Watoto

📌 Pangilia Ratiba ya Mtoto:
. Asubuhi: Shule
. Mchana: Mapumziko ya uangalizi
. Jioni: Kufanya kazi za shule, michezo salama


📌 Mfundishe Mtoto:

. Atoe taarifa kwa mzazi au mlezi
. Atambue watu salama kwa msaada
. Kutumia simu kwa dharura


📌 Weka Mazingira Salama Nyumbani:
. Funga milango salama
. Ondoa vitu hatarishi
. Weka daftari la namba muhimu

🟩 Uk. 4 - Ushirikiano na Jamii

Wazazi washirikiane na walimu, majirani na viongozi wa mitaa
Tambua mtu mzima wa kuamini kumwangalia mtoto (kama dada wa kazi, bibi n.k.)
Elimisha jamii kuhusu usalama wa mtoto kupitia kampeni za mitaani


🟩 Uk. 5 - Kwetu Inasema: Elimika. Chukua Hatua.

> Kwetu ipo bega kwa bega na jamii ya Tabora kuhakikisha mtoto wa leo ni taifa bora kesho.
Tupigie au tembelea kwetu kwa taarifa zaidi.
📞 +255 
📍Tabora, Tanzania