VIJANA WA TABORA NA UPAMBANAJI KATIKA SEKTA YA KILIMO CHA TUMBAKU 

Katika msimu wa manunuzi ya tumbaku mkoani Tabora, kundi kubwa la vijana hujitokeza kufanya kazi mbalimbali katika maghala ya kuhifadhia na kuchambua tumbaku. Kama inavyoonekana kwenye picha, vijana hawa ni wapambanaji wa kweli, wakihangaika jua na mvua kwa lengo la kujipatia kipato cha halali kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na ya familia zao.
Mara nyingi, kazi hizi huwa za muda mfupi lakini zina mchango mkubwa katika uchumi wa vijana wa Tabora. Wengi wao hutumia pesa wanazozipata kujiendeleza kielimu, kuanzisha biashara ndogondogo, au kusaidia familia zao. Hii ni ishara tosha kuwa vijana wakipewa fursa, wanaweza kubadilisha maisha yao kwa juhudi na maarifa.

Kupitia taasisi ya Kwetu, tunatambua jitihada za vijana hawa na tunajivunia kuwa sehemu ya kuwawezesha kwa elimu, hamasa na taarifa sahihi. Kaulimbiu yetu, "Elimika Chukua Hatua," inalenga kuwainua vijana kama hawa – wanaoamini katika kufanya kazi kwa bidii huku wakiwa na ndoto kubwa za mafanikio.

KWETU – Elimika. Chukua Hatua.
🌐 www.kwetu.online ingia hapa
📨kwetuonlinetz@gmail.com 
📍 Tabora, Tanzania