Hadithi ya Aisha – Mwanadada Mpambanaji
Baada ya kumaliza Diploma ya Ualimu, Aisha alitamani sana kuajiriwa serikalini. Lakini miaka ikapita bila kupata ajira. Wengi walimcheka na wengine walimkatisha tamaa, lakini yeye hakukata tamaa.
Kwa moyo wa uthubutu, aliamua kugeuza changamoto kuwa fursa. Akaanza kuuza nguo kwa mfumo wa kukopesha (mali kauli), huku akiheshimu wateja wake, kutunza nidhamu ya fedha na kufanya kazi kwa bidii kubwa kila siku.
Kidogo kidogo, mtaji wake ukaongezeka. Nidhamu yake ikamjengea imani kwa wateja wengi zaidi. Leo hii, Aisha ni mjasiriamali anayemiliki duka lake la nguo Nzega mjini, na ni mfano wa msichana ambaye hakukata tamaa, bali aliamua kujitengenezea ajira.
✨ Funzo kutoka kwa Aisha:
. Changamoto si mwisho wa safari, ni mwanzo wa njia mpya.
. Nidhamu ya fedha na heshima kwa wateja ni nguzo ya mafanikio.
. Ujasiriamali ni daraja la kujitegemea na kujenga kesho bora.
👉🏾 Aisha anatufundisha kuwa ajira si lazima iwe kutoka serikalini pekee – unaweza kuibua fursa zako na kuandika hadithi yako ya mafanikio.